Bondia Japhet Kaseba leo amepima tayari
kumkabili mpinzani wake Rasco Chimwanza wa Malawi katika pambano la
ubingwa wa kimataifa.
Zoezi zima la upimaji lilisimamiwa na Anthony Ruta, Ibrahim Kamwe, Pendo
Njau na Dr. John Lugambila wa Muhimbili na kueleza kuwa mabondia
wote wapo katika hali nzuri ya ushindani.
Kaseba amejinadi kumsambaratisha
mpinzani wake katika raundi za
mapema za mchezo huo. Pia kutakuwepo na mapambano ya utangulizi kama
Juma Fundi atazipiga na Hasan Kiwale (moro best), Joseph Onyango toka
Kenya atazipiga na Seba Temba wa Morogoro, huku Issa Omar Peche boy
atakapomvaa bondia mkongwe Juma Seleman na mapambano mengineyo mengi
yatapigwa katika ukumbi huo wa DDC Magomeni Kondoa