MOURINHO ASEMA TERRY ATABAKIA NAHODHA WA CHELSEA KWA JUHUDI ZAKE.
MENEJA mpya wa klabu ya
Chelsea, Jose Mourinho amedai kuwa John Terry atabakia kuwa nahodha wa
timu hiyo na kukataa kuweka wazi kama anataka kumsajili mshambuliaji
nyota wa Manchester United, Wayne Rooney. Terry
mwenye umri wa miaka 32 alikuwa nahodha wa kikosi cha Chelsea
kilichonyakuwa mataji mawili ya Ligi Kuu nchini Uingereza wakati
Mourinho alipokuwa kocha mara ya kwanza. Lakini
pamoja na kuwa nahodha kwa muda wote huo Terry hakuwa chaguo la meneja
wa mpito Rafael Banitez kwasababu ya majeraha ya mara kwa mara
yaliyokuwa yakimsumbua katika msimu wa 2012-2013. Mourinho
amesema hana tatizo na terry kuendelea kuwa nahodha wa klabu hiyo
lakini itabidi afanye kazi ya ziada kuhakikisha anakuwa na namba ya
kudumu katika kikosi cha kwanza. KOcha
huyo mwenye maneno mengi aliendelea kusema kuwa wachezaji ambao
walikuwepo katika kipindi chake cha nyuma alichokuwepo hapo wasitegemee
mteremko kutoka kwake kwani viwango vyao ndio vitawafanya wabakie katika
kikosi chake.