SURA ya Tanzania inazidi kuchafuka katika suala la usafirishaji wa madawa haramu ya kulevya baada ya mshambuliaji wa zamani wa Simba JOSEPH KANIK kukamatwa na madawa ya kulevya kwenye uwanja wa ndege.
Mshambuliaji huyo aliyewahi kuichezea Simba mwanzoni mwa miaka ya 2000, amekamatwa na madawa ya kulevya siku tatu zilizopita kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole jijini Addis Ababa, Ethiopia.