Na Mwandishi wetu
Kijana
mmoja mkazi wa kitongoji cha DDC Mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya,
Mkoani Mbeya Bwana GOODSON MWASYOGE amejikuta yupo katika wakati mgumu
baada ya kuiba simu ya mfanyabiashara eneo hilo baada ya wiki moja simu
hiyo imekuwa ikilia tumboni baada ya kupigwa huchukua kama dakika kumi
na tumbo lake kuvimba.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa Bwana ASIFIWE MWAKALONGE amethibitisha kwa tukio hilo akiwa sambamba na mjumbe Bwana MOHAMMED SAID.
Wakati huo huo Kaka wa muhanga wa tukio hili Bwana DANIEL MWASYOGE akiwa na Mama mzazi Bi CHRISTINA MWAKALONGE amemtaka aliyeibiwa simu kumsamehe kijana wao kwa kosa alilolifanya naye amekiri kutenda tukio hilo na anaomba msamaha kuwa abilisi alimpitia tuu hakuwa na tabia ya wizi na baadhi ra wananchi wa mtaa huo wanashangaa.
Kijana GOODSON ni mmoja wa wafanyakazi wa Machinjioni maarufu kama Butchery Mbalizi.
Hili
jambo ni FAIDA kwani ni fundisho kwa vijana ambao hupendelea tabia ya
kusogeza mali katika jamii na kusababisha Janga la Umasikini kuendelea
kuchukua nafasi.