MSANII wa filamu na mtayarishaji pia wa filamu Bongo Simon Mwakipagata ‘Rado’ amelishutumu na kulilaumu kundi la filamu la Bongo Movie Unity kwa kukosa upendo na kushindwa kusaidia katika matatizo, Rado aliyasema hayo kufuatia hivi karibuni kupata ajali ya gari na kujikuta akijiuguza pekee yake bila kupata faraja kutoka kundi hilo wakati yeye ni katibu wa kundi hilo.
. “Siku zote mimi upenda kuwa mkweli hata kama mwingine atachukia hivi karibuni wakati narudi kutoka Location nilipata ajali na kuumia sehemu ya kifua ilikuwa ni ajali mbaya namshukru Mungu kuniponya lakini rafiki zangu wa Bongo movie hakuna hata mmoja aliyejitokeza kunijulia hali wakati walikuwa na taarifa, lakini tu hao hao wangesikia nimekufa wangekuwa wa kwanza kuunda kamati ya mazishi,”anasema Rado.
Msanii huyo nyota anadai kuwa tukio hilo ni la pili kwake kupata ajali lakini mara zote hizo amekuwa jirani na wasanii ambao alikuwa akiigiza nao katika kundi la Jumba la Dhahabu ambao ni Niva, Baga, Wema Sepetu na wasanii wengine ambao kila awapo na tatizo uwa mbele katika kumsaidia na kumfariji katika ugonjwa lakini si kundi ambalo yeye ni kiongozi pia kama katibu.