Wazazi wa Dogo Janja aka Janjaro, wamekuja Dar es salaam wiki hii kuangalia maendeleo ya mtoto wao baada ya kusikia tetesi kuwa anarudi Tip Tipo Connection na kuhisi Watanashati wameshindwa kumsimania.
Ostaz Juma kushoto,wazazi wa Dogo Janja katikati na Dogo Janja wa mwisho Wakiongea na Bongo5 jana wakiwa katika Hotel ya Atrium, Sinza jijini Dar es salaam, Baba wa Dogo Janja, Mzee Chende alisema waliamua kusafiri kutoka Arusha mpaka Dar ili kukutana na mmiliki wa Watanashati Ostaz Juma, ili wajue kimetokea nini kwa mtoto wao.
Wazazi wa Dogo Janja “Tuna week moja, mimi na mke wangu tumetoka Arusha kukutana Ostaz Juma ili tujue nini kilitokea baada ya kusikia Dogo Janja anataka kururi Tip Top, sasa tumekuna na Ostaz Juma tumeongea tumekuta mtoto wetu hana tatizo lolote na yupo salama kwa Watanashati na tumejua yalikuwa mambo ya kuzusha tu,” alisema baba yake na Janjaro. Kwa upande wake mmiliki wa kampuni ya Watanashati
Entertainment, Ostaz Juma na Musoma alisema ni kweli wazazi wa msanii huyo waliingiwa na wasiwasi baada ya kusikia rapper huyp anataka kurudi Tip Tip kwa kujua Watanashati imemtelekeza.
Ostaz Juma na Dogo Janja “Ingawa mawasiliano ya simu yalikuwepo lakini walitaka kuja tukae pamoja wote ili tuongee. Sisi kama Watanashati tulikaa nakuamua tuwaite wazazi wa Dogo Janja tukae nao ili tuzungumze na kweli tumefanikiwa kuwaleta tumeongea nao na hakuna tatizo na tumepiga nao picha za ukumbusho,” alisema Ostaz. Dogo Janja alisema amefurahishwa na kitendo cha wazazi wake kuja ili kujua maendeleo yake huku akiwaahidi wazazi wake kuwatembeza sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam ili ‘waielewe mitaa’ (Kwa sauti ya Fid Q).
Ostaz Juma kushoto,Wazazi wa Dogo Janja katikati na Dogo Janja wa mwisho