Muigizaji wa filamu za kibongo maarufu kwa jina Jackline Wolper amewaasa waigizaji wenzake wa kike kuacha kuvaa nguo za nusu uchi kwani ni kinyume na mila na tamaduni za kitanzania .
Wolper aliyasema hayo kufuatia kupigiwa kura na kushinda kama muigizaji wa kike mwenye muonekano wa kistaa...
Akizungumza katika kipindi cha filamu cha Take One kinachorushwa Clouds Tv , Wolper alisemakuwa yeye hawezi kuvaa mavazi ya nusu uchi ila anavaa mavazi yanayomsitiri mwili wake na bado anapendeza kuliko hao wanaovaa nusu uchi halafu hawapendezi.
"Nawashukuru sana mashabiki wangu kwa kunipigia kura hadi kuibuka mshindi, na ni kweli najiamini kwa kuwa mimi hata siku moja huwezi kuniona nimevaa nguo za nusu uchi kama wengine" Wolper