Bibi harusi wa miaka nane huko
yemen,amefariki dunia kutokana na michubuko ya ndani aliyoipata usiku wa
harusi yake,alitoka damu mpaka kufa baada ya uke wake kutanuka
kulikosababishwa na kufanya mapenzi na mume wake mwenye miaka 40.
Mtoto aliyejulikana kwa jina la
Rawan,alifariki huko Hajjah,Yemen kutokana na ripoti tulizonazo mtoto
huyo alifariki jumapili,septemba 8.
Raia wema sehemu hiyo wanataka kukomesha
suala hilo la kuoa wasichana wadogo na waliwaita polisi kuwakamata mume
wa yule mtoto aliyefariki na familia yake. Lakini bado ndoa za
wasichana wadogo za kulazimisha huko Yemen zinabaki kuwa utamaduni
unaokubalika na jamii kwenye vijiji vingi.
Raia hao waliwaita polisi kuja
kuwakamata huyo mume mkatili na familia ya mtoto na kuwapeleka kortini
ambako haki itatendeka na kesi hiyo itawasaidia kukomesha uoaji wa
wasichana wadogo kwenye nchi yao. Bloggers wa Kuwait wamemuombea 'bibiharusi' na kumlaani 'bwanaharusi' wakisema ni mnyama mkatili anayetakiwa kuadhibiwa vikali.
Al Bawaba inaripoti kuwa zaidi ya robo ya wasichana wadogo huko Yemen wanaolewa kabla ya umri wa miaka 15. Inaongeza kuwa nchi hiyo ilipitisha
sheria februari 2009 ambayo iliweka umri wa chini kabisa kuolewa ni 17
lakini hiyo ilikataliwa baada ya watengenezaji wa sheria kusema kuwa sio
ya kiislamu.
Mwaka 2010 msichana wa miaka 13
aliyelazimishwa kuolewa alifariki siku tano baada ya harusi yake
kwasababu alipata mpasuko wa ndani kutokana na kufanya mapenzi ,ilisema
organisation ya haki za binadamu ya eneo hilo.
Chanzo cha world vision kilichotolewa machi kinasema watoto wengine wengi wanaolewa kutokana na umaskini na majanga.
Wazazi ambao wanaishi kwa uoga wa
majanga ya asili,vita na kuharibika kwa uchumi huwa wanakimbilia ndoa za
aina hiyo kuokoa familia zao.
Kila siku wasichana 39,000 chini ya umri wa miaka 18 wanaolewa,kilisema chanzo cha World Health Organization.
|