So Rehema Chalamila aka Ray C na mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds TV, Zamaradi Mketema haziivi? Katika kile kilichoacha wazi midomo ya watu wengi, warembo hao leo wameingia kwenye vita vya maneno kwenye mtandao wa Instagram. Alianza Zamaradi aliyepost picha yenye maneno ya mafumbo:
Picha hiyo aliiandikia maneno haya:
Huwezi amini sikuchukii ila nimezidi kukudharau!!!! Katika watu wa mwisho kabisa ambao siwezi kupanic nao hata siku moja ni WEWE.. Dont waste your energy.. you have so much to accomplish ndugu.. mi hunipi tabu kabsa, kabsaa, kabisaaaaaaaaa yani sanasana unanichekesha tu na vituko visivyoisha.. lol!! Ila sikulaumu sana sio kosa lako maskini…
ungekuwa una akili usingefanya hayo ya kitoto tena hasa KWA KIPINDI HIKI.. na huenda hiyo sio akili yako mwaya.. NIMEKUSAMEHE BURE maana hapo ulipo hujielewi bado..
Dramas Dramas Dramas… sizipendagi ila huwa zinanifata zenyewe.. lol!!! Mbona naandamwaga hivi jamani kwani kosa langu nini mimi mtoto wa watu… hahahahahaaaa majanga haya @wemasepetu anyways sorry to my good people jamani kwa mapost ya aina hii..
Dramas Dramas Dramas… sizipendagi ila huwa zinanifata zenyewe.. lol!!! Mbona naandamwaga hivi jamani kwani kosa langu nini mimi mtoto wa watu… hahahahahaaaa majanga haya @wemasepetu anyways sorry to my good people jamani kwa mapost ya aina hii..
sometimes inabidi coz mwisho wa siku mi ni binaadamu tu wa kawaida.”
Wema naye aliongeza kwa kuchangia: Mbona majanga….. dont waste ur tym to fools maamy…. nawe utaonekana a fool… fanya yako… wanaokufatilia wanatamani wawe kama wewe… na si kingine its called ENVY.”
“Sina hata time nae mammy bado ana vichembechembe kwenye ubongo.. maana ghafla tu anaanza kuniparamia jamani.. lol!!! Kishafulia anatafuta kick kwa kugombana na watu.. mtu wa zamani,” aliongeza Zamaradi.
Japokuwa Zamaradi hakutaja wazi nani mlengwa wa ujumbe huo, ni Ray C mwenyewe ndiye aliyejibu kwenye maelezo ndani ya post yake kwenye mtandao huo akisema:
“Hihihi kazi kwelikweli mi naweza posts zangu watu wanajihisi au wanaumia. Tatizo skuliiiii shauri yako #uki skuli kdg wala matatizo hakuna ila km huja skuliii mweeeh unakua mbulula mama we hujui fanya yako achana na watu weusi,” aliandika Ray C.
Aliongeza tena, “Haswa anajiona kichwa kumbe mbulula haswaa Hana lolote,Watu wameanza shughuli hizo anazofanya wenzie tulishazifanya kitambooooooooo,tushauza sura sanaaaaaaaaaa zaid ya miaka. 12 namuangalia simmalizi maana haeleweki.”
Haukuishia hapo, Zamaradi aliongeza tena kwa kuweka post mpya.
“Nashusha sana hadhi yangu kwakweli dealing with watu wenye hasira na maisha ya watu wengine… this is not ME kabisa. Una mengi ya kutukaniwa lkn mi ni binaadamu ninaejua baya na zuri.. maisha yashakushinda wewe sasa USIPANIC.. jipange. Ushafanywa yote ya dunia ntakuweza wapi mie mtu wa zamani,” aliandika Zamaradi kwenye picha hiyo.