Mrembo Yusta Mkali, mkazi wa Kawe, Dar ambaye alikuwa mke wa mtu
anadaiwa kuuawa kwa kutobolewa koromeo na mumewe, Musa Senkando na
kusababisha simulizi ya kutoa machozi kisa kikielezwa kuwa ni wivu wa
kimapenzi.
Polisi wa kituo cha Kawe wakiukagua mwili wa marehemu Yusta.
Mtuhumiwa wa mauaji, Musa Senkando.
Mwili wa marehemu Yusta ukipelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.
Wakazi wa Kawe wakiwa na simanzi wakati mwili wa marehemu ukipelekwa hospitali.
“Huu ni unyama wa ajabu sana. Haya mapenzi ni ya kuyatazama sana.
Ona sasa mwanaume amemuua mkewe. Inauma sana,” alisema mama Jack ambaye
ni jirani wa familia hiyo.
Ilikuwa ni simanzi na majonzi wakati wa kuaga mwili wa marehemu
Yusta, jana katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar kabla ya
kuusafirisha kwenda mkoani Dodoma kwa mazishi.