MTU
mmoja aliyefahamika kwa jina la Tiger Mwaigomole (70) Mkazi wa kata ya Masukulu
wilayani Rungwe amefariki dunia ghafla akiwa katika chumba cha Mahakama ya
Wilaya ya Rungwe akifuatilia mwenendo wa kesi inayomkabili mtoto wake wakati
Mahakama ikiendelea.
Tukio
hilo la aina yake lilitokea hivi karibuni majira ya saa 9 alasiri ndani ya
Mahakama hiyo ambapo Marehemu alifika mahakamani hapo akiwa na mwanaye
aliyejulikana kwa jina la Lusajo Tiger (40) wakiwa na lengo la kumwekea dhamana
ndugu yao Gwakisa Tiger ambaye alifikishwa mahakamani hapo akituhumiwa kwa kosa
la kupigana na kujeruhi katika ugomvi uliotokea kijijini kwao.
Kwa
mujibu wa mtoto wa Marehemu aliyekuwa ameongozana nae Mahakamani hapo Lusajo
Tiger alisema wakati kesi ikiendelea chini ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya
Rungwe, Kingwele, ndugu yao alipandishwa kizimbani kusomewa mashtaka
yanayomkabili ndipo marehemu alipoanza kutetemeka kwa madai kuwa anajisikia
baridi kali sana.
Alisema
kutokana na marehemu kulalamikia baridi aliamua kumnunulia chai ya moto ili
anywe na kupunguza baridi ambapo baada ya kufanya hivyo marehemu alikata roho
muda mfupi baada ya kumaliza kunywa chai aliyokuwa amepelekewa huku akiwa
amekaa ndani ya chumba cha mahakama hiyo.
Kutokana
na tukio hilo Askari polisi waliokuwepo mahakamani hapo waliuchukua mwili wa
marehemu na kuukimbiza katika Hospitali ya Wilaya ya Rungwe Makandana kwa ajili
ya vipimo lakini hata hivyo mwili ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu
za mazishi ingawa ripoti ya kifo chake haikutolewa mapema.
Wakati
huo huo Hukumu ya kesi ya mauaji dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Rungwe, John Mwankenja inayowakabili Hakimu Mwakalinga na wenzie watatu
huenda ikatolewa Novemba 11 mwaka huu baada ya Mahakama kuu kanda ya Mbeya chini
ya Jaji Samwel Karua kumaliza kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka pamoja
na utetezi kwa upande wa watuhumiwa.
Kwa mujibu wa Jaji Karua alisema baada
ya kumaliza kusikiliza pande zote mbili atatumia muda wa siku mbili kwa ajili
ya kuandika hukumu ambayo itaitoa Novemba 11, Mwaka huu, kesi ambayo inasimamiwa
na Mwanasheria wa Serikali Archiles Mulisa huku watuhumiwa wakitetewa na
M