Filamu mpya ya Vincent
Kigosi aka Ray aliyoigiza na aliyewahi kuwa mpenzi wake na Mr. Blue,
Najma, ambaye pia ni mwanamuziki, imeingia sokoni, Oct 29.
Fan’s Death imetengenezwa na kampuni RJ na inasambazwa na kampuni ya
Steps Entertainment ambapo pia muigizaji Rammy Galis aliyewahi kuigiza
filamu ya 'Malaika' atakuwemo.
Najma aliwahi kutamba na wimbo wake 'Don't Let Me Go' aliomshirikisha Mr
Blue, pia alionekana kwenye video ya 'Tabasamu'.