Clouds Media leo hii wamethibitisha kuwaleta wasanii zaidi ya watatu
kutoka nje ya Tanzania (International artist), na leo hii wamethibitisha
kudondoka kwa msanii kutoka
Nigeria Davido anaefanya poa sana Africa na single kadhaa kali, ikiwemo Gobe.
msikilize davido akiongea mwenyewe kutangaza ujio wake
Wasanii zaidi ya 40 kutoka Tanzania watapanda jukwaa hilo la Fiesta na
leo hii imetoka list ya wachache tu wakiambatana na Davido ambao ni
Afande Sele, Makomando, Mr Blue, Young Killer, Young D, G Nako, Joe
Makini, Nikki wa pili, Kala Jeremiah na Chidi Benz, list itaendelea siku
ya kesho ambapo utamsikia msanii mwingine wa nje atakae tua bongo
pamoja na muendelezo wa list ya wasanii wa hapa hapa.
Fiesta itarajiwa kufanyika siku ya jumamosi ya tarehe 26 ndani ya viwanja vya leaders.