“Ilikuwa ni baada ya kugongewa pasipoti yangu nikaingizwa kwenye kitengo cha polisi wa madawa ya kulevya ambao walinitaka nivue nguo zote ili nikaguliwe,” alisema kwa masikitiko.
Msanii huyo alisema mbaya zaidi siku hiyo alikuwa katika mzunguko wake wa mwezi lakini maofisa hao hawakujali.
Kama vile haitoshi, Devota alisema kuwa, baada ya kumalizika kwa zoezi hilo maofisa hao walimchezea sehemu za kifuani huku wakimwambia kama hakutaka kufanyiwa hivyo angerudishwa alikotoka.
“Kwa kweli nimeumia sana kwa kitendo nilichofanyiwa, nimeshinda nikilia kutwa nzima na kila nikikumbuka naumia,” alisema Devota.