Baraka Da Prince kayatoa ya moyoni waliosema ameshindwa kuongea kiingereza

Kama utakuwa unakumbuka hivi karibuni msanii wa Bongo Fleva, Baraka Da Princekutoka kwenye label ya Rockstar 4000 aliingia kwenye headlines baada ya mpenzi wake Najma kuonekana kuwa kama mkalimani wake kwenye interview ya MTV Base.

Baraka Da Prince na kuyaongea ya moyoni>> Unajua watanzania asilimia kubwa wanakuwa wanakurupuka sana mimi sijaona kwanza kitu cha ajabu cha mimi kutumia lugha ya Kiswahili, mimi nimeenda MTV Base nimeulizwa Je unataka kutumia lugha gani ili uwe huru nikawajibu ninaweza nikatumia lugha ya Kiingereza lakini sitokuwa huru’

‘Sasa wabongo walifurahi wengine wakasema nimeshindwa kuongea kingereza kwangu mimi nimeitangaza  lugha yangu ya kiswahili halafu Najma hakuwa mkalimani wangu mimi bali alikuwa anawambia yule mtangazaji kile ninachokizungumza mimi’- Baraka Da Prince

Unaweza ukabonyeza play kumsikiliza Baraka Da Prince akitoa ya moyoni kuhusu waliosema ameshindwa kuongea kingereza

Share this post :
https://www.facebook.com/hassani.haji

Follow me on instagram

https://www.instagram.com/hancyclassics/

Follow Me Insta

A photo posted by hancyb (@hassanaly_b) on

 
Support : hassani bakari haji | +255755537543 | +255712919980
Copyright © 2016. hancyclassics - All Rights Reserved
Template Created by hassani bakari Published by hassani bakari
Proudly powered by hassani