PICHA: Yanga imefufua matumaini ya kucheza nusu fainali ya CAF, kwa kuvunja rekodi yao mbaya

Baada ya kucheza mechi zake nne bila ushindi wowote kwa wawakilishi pekee wa Tanzaniakatika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika Yanga, August 13 2016 ilikuwa ni nafasi yao ya mwisho kuweza kufufua matumaini ya kuwania kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kwa kucheza dhidi ya MO Bejaiaya Algeria.

Yanga ambao walikuwa na point moja katika msimamo wa Kundi A lenye timu za Medeamaya GhanaTP Mazembe ya Congo na MO Bejaia ya Algeria, walikuwa wanatakiwa kuibuka na ushindi wa aina yoyote ili waweze kufufua matumaini, hata hivyo Yanga ambao hawajawahi kupata ushidni wowote katika hatua ya Makundi toka mwaka 1970 walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0.

Goli pekee la Yanga lililofufua matumaini ya safari ya nusu fainali ya michuano ya CAF, lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa waBurundi anayeichezea timu hiyo Amissi Tambwe dakika ya 4, kwa matokeo hayo Yangasasa wanatakiwa kuifunga TP Mazembeugenini na kuomba mchezo wa Medeama naMO Bejaia umalizike kwa sare yoyote ili wafuzu huku Mazembe akiifunga Medeama katika mchezo wao wa tano.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Yangahaijawahi kupata ushindi wowote katika michuano ya Kombe la shirikisho na klabu Bingwa hatua ya Makundi toka mwaka 1970, na ilikuwa imecheza jumla ya mechi 14, sare 6 na imefungwa mechi nane, ushindi wa leo waYanga wanakuwa wameandika historia na kuvunja rekodi yao ya michuano ya kimataifa.


Share this post :
https://www.facebook.com/hassani.haji

Follow me on instagram

https://www.instagram.com/hancyclassics/

Follow Me Insta

A photo posted by hancyb (@hassanaly_b) on

 
Support : hassani bakari haji | +255755537543 | +255712919980
Copyright © 2016. hancyclassics - All Rights Reserved
Template Created by hassani bakari Published by hassani bakari
Proudly powered by hassani