BOLT KUKABIDHI ZAWADI KWA MSHINDI WA FRENCH OPEN WANAUME.
SHIRIKISHO la Tenisi
nchini Ufaransa limetangza kuwa mshindi wa michuano ya wazi ya Ufaransa
kwa uonde wa wanaume atakabidhiwa zawadi na mkimbiaji nyota wa mbio fupi
kutoka Jamaica Usain Bolt. Bolt bingwa mara sita wa michuano ya
Olimpiki ambaye jana alishindwa kutamba katika mashindano ya Diamond
League yaliyofanyika jijini Rome baada ya kushindwa na Justin Gatlin wa
Marekani, atakuwa mwanariadha wa kwanza kupata heshima hiyo kwenye
michuano mikubwa ya tenisi. Nusu fainali kwa upande wanaume inatarajiwa
kufanyika leo ambapo bingwa mtetezi wa michuano hiyo Rafael Nadal
anatarajia kuchuana na Novak Djokovic ukifuatiwa na mchezo mwingine wa
nusu fainali kati ya Jo-Wilfried Tsonga dhidi ya David Ferrer. Kwa
upande wa wanawake ambapo fainali itafanyika Jumamosi kati ya Serena
Williams na maria Sharapova, tuzo yao itakabidhiwa na bingwa mara tatu
wa zamani wa michuano hiyo ambaye pia amewahi kuongoza katika orodha za
ubora kwa wanawake Arantxa Sanchez Vicario wa Hispania.