Wema Sepetu na Kajala Masanja. |
KASUMBA
ya wanawake wengi kuwaambia mashoga zao siri zao nzito inadaiwa
kumfanya msanii maarufu wa filamu Bongo, Wema Sepetu kufunguka kuwa,
bila kuwa karibu na Kajala Masanja itakuwa ni kama kuamua kutembea
mtupu.
Wema alifikia
hatua ya kutoa maneno hayo katikati ya wiki hii kwa kuposti picha
kwenye mtandao wa Instagram ikimuonesha yeye, meneja wake Martin Kadinda
na Kajala huku akisindikiza na ujumbe mzito uliosomeka:
“I always call my poch and I fell so naked without, I need her
everywhere with me. I hope that’s how they out each other.” Aliandika
kimombo, alimaanisha nini?
Tafsiri ya maneno hayo ni kwamba, Wema anamchukulia Kajala kama pochi
yake na bila yeye anajihisi yuko uchi kiasi kwamba anataka kila sehemu
wawe wote. Kajala amjibu Baada ya Wema kutundika ujumbe huo, Kajala naye
alijitutumua na kutupia maneno ya kumshukuru (Wema) huku akieleza kuwa,
kama ni hivyo yeye hana la kusema.
“Nimeyapenda maneno hayo, kama ni hivyo mimi sina la kusema,” aliandika Kajala kwenye mtandao huo.
Kwa nini Wema aseme hivyo?
Yawezekana Wema alimaanisha vingine lakini wachambuzi wa mambo
wamekuwa na maoni yao huku wengi wakieleza kuwa, inawezekana Wema
anasema hivyo kutokana na ukweli kwamba Kalaja anajua siri zake nyingi.
“Unajua Wema amekuwa na marafiki wengi sana lakini inavyoonekana
Kajala amemshiba sana na anajua siri zake nyingi. Wema anaposema bila
Kajala itakuwa ni kama anatembea uchi anamaanisha kuwa, wakikorofishana
kuna hatari ya kuanikana mambo yao nyeti.
“Watu
wanazusha kuwa Wema anauza ‘unga’, mara anatembea na kigogo mmoja
serikalini, ukweli wa haya anaujua Kajala na ndiyo maana amemshiba ili
siri zake ziendelee kuwa sirini,” alidai mmoja wa marafiki wa karibu wa
Kajala aliyeomba hifadhi ya jina lake.

Mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Mariam wa Kinondoni alisema:
“Hawa wana siri nzito, kila mmoja anajua mambo ya ndani ya mwenzake na
ndiyo maana hakuna ambaye yuko tayari kumtosa mwenzake, watazinguana
lakini watarudiana.” Kajala anasemaje?
Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Kajala kuzungumzia maoni yake
juu ya ujumbe huo wa Wema ambapo alisema, hana neno la kutia isipokuwa
amefarijika tu kusikia anapendwa kiasi hicho.
“Kwa kweli hata kama wewe unaambiwa hivyo lazima utafurahi sana maana
sikuwa najua kuwa napendwa na shosti wangu (Wema) ila hata mimi
nampenda sana yaani siwezi kueleza, hayo manenomaneno ya watu hatuwezi
kuyasikiliza,” alisema Kajala. Msikie Wema
“Nilichokiandika nilikimaanisha, Kajala kwa sasa siyo rafiki yangu
tena ni ndugu ambaye nampenda sana kutoka moyoni mwangu na nitampenda
siku zote na ndiyo maana sijisikii kuwa mbali naye,” alisema
Wema.Watadumu?
Swali ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza ni kama ushosti wa wawili hao
utadumu kwani mara kadhaa imekuwa ikidaiwa kuwa wametibuana na baadaye
kuonekana wako pamoja, mazingira yanayoashiria kuwa huenda siku moja
wakazinguana moja kwa moja.
Hayo yanakuja kufuatia historia ya Wema ambaye amekuwa hadumu na
marafiki zake, mfano ukiwa kwa msanii Snura Mushi (staa wa Majanga)
ambaye waliwahi kuwa marafiki kupitiliza lakini baadaye wakatosana