BATULI:NAMUOGOPA MAMA KANUMBA ..NIKIMUONA HATA KUMSALIMIA SIWEZI


Stori: Brighton Masalu Staa anayesongesha maisha yake Bongo Movies, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’ amesema akimuona mama wa marehemu, Steven Kanumba, Flora Mtegoa anaogopa hata kumsalimia kwa madai hukumbuka mambo mengi ya marehemu. Akimwaga mawili matatu mbele ya kinasa sauti chetu,  maeneo ya Kinondoni, jijini Dar, Batuli ambaye aliibuliwa na marehemu Kanumba kwenye filamu ya Fake Smile, alisema kamwe hawezi kuondoa uwepo wa marehemu katika ubongo wake na ndiyo maana anaogopa hata kumsalimia mama Kanumba.
 “Ukweli ni kwamba bado sijawa na ujasiri wa kumkabili mama huyo, huwa nakumbuka mambo mengi sana kila nikimuona, naishia kumkimbia tu, hata pale Kariakoo juzikati niliogopa kabisa kumsalimia kwani ningeishia kulia mbele ya umati,” alisema Batuli.
Share this post :
https://www.facebook.com/hassani.haji

Follow me on instagram

https://www.instagram.com/hancyclassics/

Follow Me Insta

A photo posted by hancyb (@hassanaly_b) on

 
Support : hassani bakari haji | +255755537543 | +255712919980
Copyright © 2016. hancyclassics - All Rights Reserved
Template Created by hassani bakari Published by hassani bakari
Proudly powered by hassani