PETE YA NDOA IMENIPONZA....NDOA IPO HATARINI



Wadau nipo njia panda naombeni ushauri wenu, nimefanya kosa kubwa na nalijutia Tafadhali naomba ushauri badala ya kunituhumu
Mwezi nilikuta na demu mmoja tulisoma naye chuo kitambo alikuwa demu wangu for time being, so baada ya miaka kadhaa tukaja kukuta sehemu, shetani akanipitia nikavunja amri ya sita naye
Baada ya kurudi home nikagundua sina pete, nikajaribu kukumbuka nilipoiweka sikupata majibu Baada ya siku kadhaa yule demu akzidi kunisumbua na kutaka niwe karibu naye sana lakini nikaona si vyema maana anaweza kusababisha mtafaruku kwa ndoa yangu
Baada ya kuona nampotezea akaniambia sasa unajifanya mjanja pete yako ni nayo na nahitaji sh 500,000 cash ama sivyo naharibu kwa mkeo kwamba pete ninayo na ulinikopa.
Kibaya zaidi wife aliniuliza pete umepeleka wapi nikadanganya nimeisahau ofisini nilikuwa nafungua printer sasa pete ikawa inani disturb nikaivua , nilipoenda jumatatu nikamwambia nahisi wahudumu wa usafi wameiiba maana siiona pale nimeiweka naendelea na uchunguzi.
Mwanzo nilimpuuzia lakini mshenzi yule kapeleleza hadi wife anapofanya kazi na kapata simu yake, juzi kampigia kamwambia "naomba mkumbushie mumeo deni langu mimi xxxxx nampigia simpati" halafu akakata simu. Niliporudi wife kanibana nikamwambia ni mambo ya kazi tu akataka kujua no yake kaipataje, nikazuga zuga na ubabe wa kiume yakaisha
Nikipiga akili nimuendee Polisi naona kama kitanuka na wife atajua Nikifikiria kumlipa akili hainipi kabisa....kilo tano? Sijui nimueleze wife ukweli?
Nimejaribu kumpiia simu na kumbembeleza kagoma anachohitaji ni kilo tano au aniharibie kwa wife Tafadhali ushauri wakuu lawama na madongo hayatanisaidia
Share this post :
https://www.facebook.com/hassani.haji

Follow me on instagram

https://www.instagram.com/hancyclassics/

Follow Me Insta

A photo posted by hancyb (@hassanaly_b) on

 
Support : hassani bakari haji | +255755537543 | +255712919980
Copyright © 2016. hancyclassics - All Rights Reserved
Template Created by hassani bakari Published by hassani bakari
Proudly powered by hassani