Volcano yenye ukubwa wa Ubelgiji (Belgium) imegunduliwa kwa mara ya
kwanza, na jopo la wanasayansi chini ya bahari ya Pacific. wanasayansi
hao, wamegundua kuwa mwamba huo mkubwa ulitokana na mlipuko wa lava, na
kuifanya volcano hiyo mpya kuwa sio tu ni kubwa duniani, bali ni kubwa
katika solar system-kubwa kuliko Olympus Mons (iliyoko mars.)
Tamu Massif Iko juu ya plateau kubwa iliyoko Km 2 chini ya maji,
kaskazini-kusini mwa bahari ya pacific ya mashariki ya Japan,volcano
hiyo yenye ukubwa wa sq Km 310,000 (119,000 sq m) haina madhara
wanasayansi hao wamesema. Mara ya mwisho kuripuka ilikuwa ni chini ya
maji, miaka milioni 142 iliyopita wakati wa kipindi cha mwisho cha
Jurassic, kabla binaadam kuumbwa
Utafiti uliochapishwa katika "Nature Geoscience unaonyesha kuwa
formation zaidi ya miamba mikubwa chini ya maji inaonekana kuwa ni
matokeo ya volcano kubwa zilizokufa zamani.