Nikki Miinaj, Drake na Lil Wayne waongezewa mshkaji mwinginekatika
familia yao baada ya The Game kusainiwa rasmi chini ya YMCMB siku ya
jana.
Cash Money C.E.O, Birdman ametangaza rasmi kumsaini Rapper huyo kupitia
ukurasa wake wa twitter pale alipompa big up kwa kuingia katika chama
hilo ambapo The Game nae, alitoa salut kwa timu hiyo na kupitia ukurasa
wake wa twitter.
Rpper huyo kutoka Compton, 33, aliwahi kuwa chini ya Interscope Records
na kutoa album 5 ambazo zote zilifika mpaka nafasi ya kwanza katika
chats mbali mbali ilkiwemo album ya kwanza kabisa The Documentary iliyotoka 2005.