Leo hii Rapper Kala Jeremiah amesaini mkataba na kampuni SBC kupitia
kinywaji chake cha Pepsi na kutangazwa rasmi kuwa balozi wa Pepsi
nchini, na yuko tayari kwa ajili ya kuanza kufanya kazi za kibalozi
kuanzia time hii.
namshukuru sana mungu, lakini nawashukuru sana mashabiki wangu,
kwasababu bila wao nisingeweza kuchaguliwa kuwa balozi, wale watu huwa
wanaangali unakubalikaje kwenye jamii lakini unajiheshimu vipi katika
jamii, nashukuru pia vyombo vya habari kwa kunipigania mpaka kujulikana
kwenye makampuni makubwa kama hayo.
Kala alikataa kuzungumzia mtonyo alioupata kutokana na mkaba huo na
kusema kuwa hawezi kutaja na itabaki kuwa siri yake, ila hajawahi
kusaini mkataba mnono kama huu ni kwa mara ya kwanza kusani mkataba
mnono kama huo.