AZONTO LIVE IN DAR, APAGAWISHA MASHABIKI WAKE


Fataki zilipigwa na kuruka hewani kuwashiria ufunguzi wa shoo ya Azonto ambapo mara baada ya fataki hizo Fuse ODG alipanda jukwaani hapo
 MSANII wa Ghana mwenye maskani nchini Uingereza Fuse ODG, juzi alifanikiwa kuwateka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa kufanya shoo ya kihistoria, huku akipandisha mzuka kwa mashabiki waliohudhuria shoo hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ustawi wa Jamii.
Msanii huyo anayetamba na kibao cha Azonto pamoja na Antenna aliweza kuwateka mashabiki wake baada ya kupanda jukwaani hapo na kucheza pamoja na mashabiki miondoko hiyo.

Kwa kumuunga mkono msanii huyo baadhi ya mashabiki waliohudhuria shoo hiyo walipanda jukwaani hapo na kuanza kucheza naye pamoja na kumfundisha msanii huyo miondoko ya Kiduku ambayo umezoeleka kuchezwa hapa bongo.

Msanii huyo alionekana kumudu kucheza kiduku ambapo aliungana na baadhi ya mashabiki wake waliopanda jukwaani hapo.

Shoo hiyo imeonyesha kufanikiwa kwa kuhudhuriwa na mashabiki wengi ambapo baadhi ya wasanii kutoka nyumbani walitumbuiza huku msanii Hamis Ramadhan 'H.Baba' alionyesha mashabiki wake kuwa yeye ndiye mkali wa miondoko ya Bongo Bolingo Fleva.

Shoo hiyo pia iliweza kunogeshwa na baadhi ya wasanii akiwemo Banana Zoro, kundi la Tip Top Conection akiongozwa na Madee pamoja na Tundaman ambapo walipanda jukwaani hapo pamoja na msanii wa hip hop Chid Benz.




Add caption

Share this post :
https://www.facebook.com/hassani.haji

Follow me on instagram

https://www.instagram.com/hancyclassics/

Follow Me Insta

A photo posted by hancyb (@hassanaly_b) on

 
Support : hassani bakari haji | +255755537543 | +255712919980
Copyright © 2016. hancyclassics - All Rights Reserved
Template Created by hassani bakari Published by hassani bakari
Proudly powered by hassani